Jarida la Mapishi

Wali wa karanga

Wali wa karanga | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    Dakika 30
  • Kupika
    Dakika 20
  • Walaji
    4

Wali wa karanga, ni wali mtamu na wenye harufu nzuri ambao hupikwa kwa kutumia mchele, karanga zilizo kaangwa, pamoja na viungo vya aina mbali mbali. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika wali huu wa karanga.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kontena dogo. Weka maji, kisha roweka choroko na dengu ndani ya hilo kontena lenye maji kwa muda wa dakika 30. Baada ya dakika 30, mwaga maji yote yaliyomo kwenye kontena na kubakiwa na choroko na dengu peke yake.

    Step2

    Chukua paper towel. Weka choroko na dengu juu ya hiyo paper towel ili zikauke maji.

    Step3

    Chukua sufuria la ukubwa wa wastani. Weka kwenye hilo sufuria, mchele, maji, binzari ya manjano, pamoja na chumvi, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa.

    Step4

    Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, halafu funika sufuria na uache iendelee kuchemka taratibu kwa muda wa dakika 12 mpaka 15, au hadi utakapo ona wali umeiva na maji yote kwenye sufuria yamekauka, kisha epua na uweke pembeni. Hakikisha hukorogi kabisa wali wakati unaupika.

    Step5

    Chukua kikaango kidogo na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kikaango kipate moto. Weka karanga kwenye hicho kikaango, kisha kaanga bila kutumia mafuta huku ukikoroga na kutikisa kikaango mara kwa mara kwa muda wa dakika 2, au hadi utakapo ona zimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia. Ondoa karanga hizo kwenye kikaango na uziweke kwenye kontena.

    Step6

    Weka mafuta ya kupikia kwenye kikaango hicho hicho, kisha acha mafuta yapate moto. Weka choroko pamoja na dengu, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1, au hadi utakapo ona vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step7

    Weka mbegu za haradali pamoja na majani ya mvuje, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa sekunde 30.

    Step8

    Weka karanga ulizo zikaanga, halafu kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1 zaidi, kisha epua na umimine kwenye sufuria lenye wali.

    Step9

    Nyunyizia limao kwenye hilo sufuria lenye wali, kisha changanya vizuri, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.