Jarida la Mapishi

Kuku wa uwatu

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 50
 • Walaji
  4

Kuku wa uwatu, ni kitoweo kitamu ambacho hupikwa kwa kutumia nyama ya kuku, majani mabichi ya uwatu, vitunguu maji, nyanya, pamoja na viungo. Kitoweo hiki chafaa kula pamoja na wali mweupe, wali wa brown au chapati. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika kuku wa uwatu.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka vitunguu maji kwenye hilo sufuria, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 10, au hadi utakapo ona vimeiva.

  Step2

  Weka tangawizi, vitunguu swaumu, vipande vya nyama ya kuku, chumvi, pilipili manga, pamoja na binzari ya manjano, halafu ongeza moto na uweke moto mkubwa, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 3 mpaka 5.

  Step3

  Punguza moto na uweke moto wa wastani, kisha endelea kukaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 15, au hadi utakapo ona vipande vya nyama ya kuku vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step4

  Weka majani ya uwatu, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 20, au hadi utakapo ona vipande vya nyama ya kuku vimeiva na kuwa laini. Epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *