Jarida la Mapishi

Wali wa kukaanga wa kamba

 • Maandalizi
  Dakika 20
 • Kupika
  Dakika 10
 • Walaji
  4

Wali wa kukaanga wa kamba, ni chakula kinachopikwa kwa kutumia kamba wabichi, mboga, pamoja na wali. Chakula hiki chenye utamu wa kipekee, kitakufanya uache kabisa kununua wali wa kukaanga wa kwenye hoteli. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika wali huu wa kukaanga wa kamba.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua kikaango kikubwa chenye vijiko 2 vya chai vya mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kamba kwenye hicho kikaango, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2 mpaka 3. Ondoa kamba kwenye kikaango na uweke kwenye sahani.

  Step2

  Weka vijiko 2 vya chai cha mafuta ya kupikia kwenye kikaango hicho hicho, kisha acha mafuta yapate moto. Weka vitunguu vya kijani, tangawizi, uyoga, mboga ya figili, pamoja na karoti, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 3.

  Step3

  Chukua bakuli. Weka ndani ya hilo bakuli, ute wa mayai 2 pamoja yai 1 zima, halafu piga piga mayai hayo vizuri, kisha mimina kwenye kikaango na uache yaive upande wa chini kwa muda wa sekunde 10 mpaka 20.

  Step4

  Weka maharage pamoja na wali mweupe, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1 mpaka 3.

  Step5

  Weka njegere, soy sauce, pamoja na kamba ulio kaanga, halafu changanya vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *