Jarida la Mapishi

Wali wa kijani

 • Maandalizi
  Dakika 30
 • Kupika
  Dakika 15
 • Walaji
  4

Wali wa kijani, ni chakula rahisi kupika ambacho hupikwa kwa kuchanganya mchele, mboga za majani aina spinachi zilizo kaangwa, pamoja na viungo. Chakula hiki chafaa kula pamoja na saladi yoyote ya mboga. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika wali huu wa kijani.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua kontena la ukubwa wa wastani. Weka maji, kisha roweka mchele ndani ya hilo kontena lenye maji kwa muda wa dakika 30.

  Step2

  Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, mboga ya spinachi pamoja na majani ya uwatu, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.

  Step3

  Chukua sufuria kubwa. Weka mchanganyiko ulio usaga kwenye hilo sufuria, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto wa wastani kwa muda wa dakika 2 mpaka 5.

  Step4

  Weka mchele, maji uliyotumia kurowekea mchele, chumvi, pamoja na pilipili manga, halafu koroga vizuri, kisha weka moto mkubwa na uache ichemke.

  Step5

  Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka taratibu kwa muda wa dakika 10 mpaka 15, au hadi utakapo ona wali umeiva na maji yote kwenye sufuria yamekauka. Hakikisha hukorogi kabisa wali wakati unaupika.

  Step6

  Wali ukishaiva zima jiko na uache utulie kwa muda wa dakika 5, ukiwa bado juu ya jiko. Baada ya dakika 5, pakua pilau kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *