Jarida la Mapishi

Biriani ya biringanya

 • Maandalizi
  Dakika 30
 • Kupika
  Saa 1
 • Walaji
  4

Biriani ya biringanya, ni chakula kitamu ambacho chafaa kupika hasa katika kipindi cha kiangazi. Chakula hiki hupikwa kwa kutumia mchele, biringanya, vitunguu maji, nyanya, nazi, pamoja na viungo mbalimbali. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika biriani hii ya biringanya.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua kontena la ukubwa wa wastani. Weka maji, kisha roweka mchele ndani ya hilo kontena lenye maji kwa muda wa dakika 30.

  Step2

  Chukua kikaango kidogo na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kikaango kipate moto. Weka nazi iliyokunwa kwenye hicho kikaango, halafu kaanga bila kutumia mafuta huku ukikoroga na kutikisa kikaango mara kwa mara kwa muda wa dakika 1 mpaka 2, au hadi utakapo ona imebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia, kisha epua na uweke pembeni ili ipoe.

  Step3

  Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, nazi uliyo ikaanga, vitunguu swaumu, tangawizi, pamoja na vitunguu maji, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.

  Step4

  Weka mbegu za giligilani, garam masala, pamoja na binzari ya manjano, kisha endelea kusaga hadi utakapo ona mchanganyiko huo wote umechanganyika vizuri.

  Step5

  Chukua sufuria kubwa lenye vijiko 2 vya chakula vya mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria mchanganyiko ulio usaga, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona imebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step6

  Weka biringanya, nusu ya chumvi, pamoja na ½ kikombe cha tui la nazi, halafu koroga vizuri, kisha weka moto mkubwa na uache ichemke kwa muda wa dakika 3.

  Step7

  Punguza moto na uweke moto wa wastani, halafu funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 15 mpaka 20, au hadi utakapo ona biringanya zimeiva na kuwa laini, kisha epua na uweke pembeni kwenye kontena.

  Step8

  Rudisha sufuria kwenye jiko. Weka kijiko 1 cha chakula cha mafuta ya kupikia kilichobaki, kisha acha mafuta yapate moto. Weka nyanya, majani ya minti, pamoja na majani ya giligilani, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2, au hadi utakapo ona mchuzi umekuwa mzito.

  Step9

  Weka mchele, maji uliyotumia kurowekea mchele, nusu ya chumvi iliyobaki, pamoja na vikombe 1½ vya tui la nazi lililobaki, halafu koroga vizuri, kisha weka moto mkubwa na uache ichemke.

  Step10

  Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka taratibu kwa muda wa dakika 10, au hadi utakapo ona maji yote kwenye sufuria yamekauka ila wali haujaiva. Hakikisha hukorogi kabisa wali wakati unaupika.

  Step11

  Ondoa nusu ya wali uliomo kwenye sufuria na uweke pembeni kwenye kontena.

  Step12

  Weka mchanganyiko wa biringanya ulioupika juu ya wali uliobaki kwenye sufuria, kisha sambaza vizuri.

  Step13

  Weka wali uliomo kwenye kontena juu ya mchanganyiko wa biringanya, kisha sambaza vizuri.

  Step14

  Nyunyizia limao juu ya huo wali, halafu funika sufuria, kisha pika biriani hiyo kwa muda wa dakika 10 mpaka 15.

  Step15

  Nyunyizia garam masala halafu changanya vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *