Jarida la Mapishi

Mchuzi wa mbuzi

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Saa 1 Dk. 15
 • Walaji
  4

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua bakuli ndogo. Weka mtindi, kisha roweka zafarani ndani ya hilo bakuli lenye mtindi.

  Step2

  Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, mdalasini, pilipili manga, iliki, majani ya mbei, karafuu pamoja na binzari nyembamba, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2.

  Step3

  Weka vitunguu maji, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 10 mpaka 12, au hadi utakapo ona vitunguu hivyo vimeiva.

  Step4

  Weka tangawizi, vitunguu swaumu, nyama, mbegu za giligilani, pamoja na chumvi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 10, au hadi utakapo ona nyama imebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step5

  Weka maji na ukoroge vizuri, kisha acha ichemke katika moto mkubwa kwa muda wa dakika 5. Baada ya dakika 5, punguza moto na uweke moto wa wastani, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 40, au hadi utakapo ona nyama imeiva.

  Step6

  Weka garam masala na ukoroge vizuri, halafu acha ichemke kwa muda wa dakika 5 zaidi, kisha epua na uweke pembeni.

  Step7

  Mimina mchanganyiko wa mtindi na zafarani kwenye hilo sufuria lenye nyama, kisha koroga vizuri, tayari kwa kula.

  Conclusion

  Kabla ya kutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *