Jarida la Mapishi

Wali wa binzari ya manjano

 • Maandalizi
  Dakika 30
 • Kupika
  Dakika 15
 • Walaji
  4

Wali wa binzari ya manjano (Wali wa manjano), ni chakula rahisi kupika, ambacho unaweza kukipika kwa muda mfupi sana wa ndani ya dakika 30 tu. Wali huu hupikwa kwa kutumia mchele pamoja na viungo mbalimbali kama vile binzari ya manjano. Wali huu wafaa kula pamoja na mboga, kuku wa kuchoma, au mishikaki. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika wali huu wa binzari ya manjano.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua kontena la ukubwa wa wastani. Weka maji, kisha roweka mchele ndani ya hilo kontena lenye maji kwa muda wa dakika 30.

  Step2

  Chukua sufuria la ukubwa wa wastani. Weka kwenye hilo sufuria, mchele, maji uliyotumia kurowekea mchele, binzari ya manjano, chumvi, pilipili manga, pamoja na iliki, halafu koroga vizuri, kisha weka moto mkubwa na uache ichemke.

  Step3

  Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka taratibu kwa muda wa dakika 10 mpaka 15, au hadi utakapo ona wali umeiva na maji yote kwenye sufuria yamekauka. Hakikisha hukorogi kabisa wali wakati unaupika.

  Step4

  Wali ukishaiva zima jiko na uache utulie kwa muda wa dakika 5, ukiwa bado juu ya jiko. Baada ya dakika 5, pakua pilau kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *