Jarida la Mapishi

Pilau ya nyama ya kusaga

Pilau ya nyama ya kusaga | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    Dakika 15
  • Kupika
    Dakika 50
  • Walaji
    4

Pilau ya nyama ya kusaga, ni chakula kitamu ambacho hupikwa kwa kutumia, wali mweupe uliopikwa, nyama iliyosagwa, mtindi, pamoja na viungo mbalimbali. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika pilau hii ya nyama ya kusaga.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua sufuria kubwa na uliweke kwenye jiko lenye moto mkubwa, kisha acha sufuria lipate moto. Weka kwenye hilo sufuria, nyama ya kusaga, binzari nyembamba, binzari ya manjano, vitunguu maji, nyanya, mbegu za giligilani, majani ya uwatu, garam masala, chumvi, tangawizi, pamoja na vitunguu swaumu, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda dakika 2 mpaka 3.

    Step2

    Punguza moto na uweke moto wa wastani, kisha endelea kupika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 25 mpaka 30, au hadi utakapo maji maji yote yamekauka na nyama imebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step3

    Mimina mtindi taratibu huku ukikoroga, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5.

    Step4

    Punguza moto na uweke moto mdogo. Weka wali mweupe uliopikwa pamoja na majani ya giligilani halafu koroga vizuri, kisha funika sufuria na upike pilau hiyo kwa muda wa dakika 5 mpaka 7.

    Step5

    Epua pilau na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Conclusion

    Kabla ya kutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.