-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 55
-
Walaji4
Mchuzi wa kuku, ni pishi lenye ladha tamu ambalo hupikwa kwa kutumia nyama ya kuku, mtindi, vitunguu maji, nyanya, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika, mchuzi huu wa kuku.
Ingredients
Directions
Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, vitunguu swaumu, tangawizi, pamoja na vitunguu maji, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini. Ondoa mchanganyiko huo kwenye mashine ya kusaga, na uweke pembeni kwenye kontena.
Weka kwenye hiyo hiyo mashine ya kusaga, nyanya pamoja na majani ya giligilani, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini. Ondoa mchanganyiko huo kwenye mashine ya kusaga na uweke pembeni kwenye kontena jingine.
Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, majani ya mbei, iliki, pamoja na mdalasini, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa sekunde 30.
Weka mchanganyiko wa vitunguu maji ulio usaga, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 7, au hadi utakapo ona mchanganyiko huo umebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.
Weka mchanganyiko wa nyanya ulio usaga, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara mwa mara kwa muda wa dakika 7, au hadi utakapo ona mchuzi umekuwa mzito.
Weka mbegu za giligilani, binzari nyembamba, garam masala, binzari ya manjano, chumvi, pamoja pilipili manga, kisha koroga vizuri.
Mimina mtindi huku ukikoroga, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara, hadi utakapo ona mtindi umechanganyika vyema pamoja na mchanganyiko wa viungo.
Weka vipande vya nyama ya kuku, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona vipande hivyo vya nyama ya kuku vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.
Mimina maji halafu koroga vizuri, kisha funika sufuria na uache ichemke kwa muda wa dakika 5.
Punguza moto na uweke moto wa wastani, halafu acha iendelee kuchemka huku ukivigeuza vipande vya nyama ya kuku mara kwa mara kwa muda wa dakika 30, au hadi utakapo ona vimeiva na mchuzi umekuwa mzito, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Conclusion
Kabla ya kutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.
Leave a Review