Jarida la Mapishi

Supu ya viazi

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 45
 • Walaji
  4

Supu ya viazi, ni supu tamu na rahisi kupika ambayo yafaa kunywa pamoja na familia nzima. Supu hii yaweza kupikwa kwa kutumia viazi mviringo au vaizi vitamu. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika supu hii ya viazi.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria maji, viazi pamoja na chumvi, kisha chemsha kwenye jiko lenye moto wa wastani hadi utakapo ona viazi vimeiva. Epua na uweke pembeni ili vipoe. Menya naganda ya viazi hivyo, kisha vikate katika vipande vidogo vidogo.

  Step2

  Chukua sufuria jingine kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka mbegu za haradali pamoja na vitunguu maji, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona vitunguu maji vimeiva.

  Step3

  Weka tangawizi, majani ya mvuje, majani ya minti, pamoja na majani ya giligilani, kisha kaanga kwa muda wa dakika 1.

  Step4

  Weka mbegu za giligilani, chumvi pamoja na viazi, kisha kaanga huku ukiroga mara kwa muda wa dakika 8 mpaka 10, au hadi utakapo ona viazi vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step5

  Weka vikombe 2 vya maji, kisha acha ichemke katika moto mkubwa. Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, kisha funika sufuria halafu acha iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona viazi vimeanza kuwa rojo. Epua na uweke pembeni ili ipoe.

  Step6

  Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, mchanganyiko wa viazi ulio upika, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vyema na kuwa laini. Ondoa mchanganyiko huo kutoka kwenye mashine ya kusaga, na uweke kwenye kontena kubwa.

  Step7

  Weka kwenye hilo kontena, mtindi pamoja na pilipili manga halafu koroga vizuri, kisha funika kontena na uliweke kwenye friji kwa muda wa saa 2, kabla ya kula.

  Conclusion

  Kabla ya kuutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *