Jarida la Mapishi

Supu ya maharage

 • Maandalizi
  Dakika 30
 • Kupika
  Dakika 50
 • Walaji
  4

Supu ya maharage, ni supu tamu na rahisi kupika. Supu hii hupikwa kwa kutumia maharage mekundu, mtindi, nyanya, tomato sauce, pamoja na viungo. Supu hii yafaa sana kunywa jioni pamoja na chakula chochote cha jioni. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika supu hii ya maharage.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua sufuria ndogo. Weka kwenye hilo sufuria maharage, maji, pamoja na chumvi, kisha chemsha kwenye jiko lenye moto wa wastani kwa muda wa dakika 30, au hadi utakapo ona maharage yameiva.

  Step2

  Chukua sufuria la ukubwa wa wastani lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, binzari nyembamba pamoja na vitunguu maji, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 3, au hadi utakapo ona vitunguu maji vimeiva.

  Step3

  Weka tangawizi, vitunguu swaumu pamoja na nyanya, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5 mpaka 7, au hadi utapo ona maji maji yote ya nyanya yamekauka.

  Step4

  Weka mbegu za giligilani pamoja na binzari ya manjano, halafu endelea kupika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa sekunde 30.

  Step5

  Mimina mtindi taratibu huku ukikoroga, kisha acha ichemke kwa muda wa dakika 1.

  Step6

  Weka maharage, majani ya giligilani, pamoja na tomato sauce, halafu koroga vizuri, kisha acha ichemke kwa muda wa dakika 5.

  Step7

  Weka garam masala na ukoroge vizuri, kisha epua na upakue kwenye bakuli, tayari kwa kunywa.

  Conclusion

  Kabla ya kuutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *