Jarida la Mapishi

Supu ya uyoga

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 15
 • Walaji
  4

Supu ya uyoga, ni supu tamu, yenye afya na rahisi sana kupika. Upishi wa supu ya uyoga unahitaji sana uvumilivu ili uweze kupata ladha nzuri kwenye supu. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika supu hii ya uyoga.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua kikaango kidogo na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kikaango kipate moto. Weka kwenye hicho kikaango mbegu za pilipili manga pamoja na mbegu za binzari nyembamba, halafu kaanga bila kutumia mafuta huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa sekunde 30, kisha epua na uweke pembeni ili zipoe.

  Step2

  Chukua kinu. Weka ndani ya hicho kinu mbegu za pilipili manga pamoja na mbegu za binzari nyembamba ulizo zikaanga, kisha twanga hadi utakapo ona mbegu hizo zimesagika vizuri.

  Step3

  Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka liki kwenye hilo sufuria, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona liki zimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step4

  Weka uyoga pamoja na vitunguu swaumu, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 7, au hadi utakapo ona vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia. Epua mchanganyiko huo na uweke pembeni ili upoe.

  Step5

  Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga mchanganyiko wa uyoga ulio upika, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vyema na kuwa laini.

  Step6

  Chukua kontena kubwa. Weka ndani ya hilo kontena, mtindi, maziwa, mchanganyiko wa uyoga ulio usaga, limao, mchanganyiko wa binzari nyembamba na pilipili manga, pamoja na chumvi, kisha koroga vizuri.

  Step7

  Funika vizuri kontena hilo, kisha liweke kwenye friji kwa muda wa saa 2, kabla ya kula.

  Conclusion

  Kabla ya kuutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *