Jarida la Mapishi

Supu ya nyama

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Saa 1
 • Walaji
  3

Supu ya nyama, ni pishi tamu, lenye virutubisho vingi na rahisi kupika, ambalo unaweza kupika kwa kutumia nyama yoyote ile uipendayo, iwe ni nyama ya ng'ombe, nyama ya mbuzi au nyama ya kondoo. Supu hii inachukua muda wa saa 1 kupika. Fuata hatua zifuatazo, ili kujifunza jinsi ya kupika supu hii ya nyama.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria, nyama, majani ya giligilani, pilipili hoho, vitunguu maji, pilipili manga, chumvi, karafuu, majani ya mbei, karoti, tanipu, mbegu za giligilani, mdalasini, vitunguu swaumu, iliki, maji, pamoja na tangawizi, halafu koroga vizuri, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa.

  Step2

  Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke motowa wastani, halafu funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa saa 1, au hadi utakapo ona nyama imeiva, kosha epua supu na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *