Jarida la Mapishi

Supu ya kabichi

Supu ya kabichi | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 40
  • Walaji
    8

Supu ya kabichi, ni supu tamu na rahisi kupika ambayo hupikwa kwa kutumia kabichi, mboga mchanganyiko, viazi, kitunguu maji, nyanya, limao, pamoja na viungo. Supu hii yafaa kunywa katika msimu wa baridi. Waweza kuipika supu hii katika muda mfupi sana wa ndani ya dakika 40 tu. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika supu hii ya kabichi.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka vitunguu maji kwenye hilo sufuria, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5.

    Step2

    Weka viazi mviringo, mboga mchanganyiko, kabichi, spinachi, pamoja na nyanya, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5.

    Step3

    Mimina maji hakafu koroga vizuri, kisha weka moto mkubwa na uache ichemke.

    Step4

    Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 15, au hadi utakapo ona mboga zimeiva.

    Step5

    Weka majani ya mvuje, pilipili manga, majani ya giligilani, garam masala, chumvi, majani ya minti, pamoja na limao halafu koroga vizuri, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 15 zaidi. Epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.