Jarida la Mapishi

Supu ya samaki

Supu ya samaki | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    Dakika 10
  • Kupika
    Dakika 20
  • Walaji
    4

Supu ya samaki, ni supu rahisi kupika kwa sababu supu hii, inapikwa kwa kutumia mahitaji ambayo ni rahisi kupatikana mahali popote ulipo. Unaweza kuongeza krimu au majani ya mrehani wakati unapika supu hii, ili kuifanya iwe tamu zaidi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika supu hii.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua samaki na uwasafishe vizuri. Chukua sufuria kubwa. Weka ndani ya hiyo sufuria hao samaki, maji, binzari ya manjano pamoja na vitunguu swaumu, kisha weka hilo sufuria kwenye jiko lenye moto mkubwa. Maji yakianza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, kisha funika sufuria na acha samaki wachemke kwa muda wa dakika 5 mpaka 7, au hadi utakapo ona samaki wameiva. Samaki wakishaiva, epua sufuria na uweke pembeni.

    Step2

    Chukua sufuria dogo. Weka ndani ya hilo sifuria mafuta ya kupikia, kisha weka sufuria hilo kwenye jiko lenye moto wa wastani na uache mafuta yapate moto. Weka vitunguu maji, na ukaange hadi utakapo ona vitunguu hivyo vimebadilika rangi na kuwa na rangi nyeupe. Weka giligilani na ukaange kwa muda wa dakika 1. Weka nyanya na uzipike kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona nyanya zimeiva.

    Step3

    Mimina mchanganyiko huo uliopika, kwenye sufuria kubwa ulilotumia kuchemsha samaki. Weka limao ndani ya hilo sufuria, kisha koroga vizuri. Weka sufuria hilo kubwa kwenye jiko lenye moto wastani, na uache supu ichemke kwa muda wa dakika 5.

    Step4

    Weka chumvi pamoja na pilipili manga, kisha koroga vizuri, halafu epua supu na upakue kwenye bakuli, tayari kwa kunywa.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.