Jarida la Mapishi

Curry powder

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 5
 • Walaji
  1

Curry powder, ni mchanganyiko wa viungo, ambayo asili yake ni kutoka nchini India. Curry powder husiadia kuongeza ladha kwenye chakula na waweza kuitumia kwenye chakula cha aina yoyote ile kama vile supu, mchuzi, saladi, n.k. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza curry powder hii kwa ajili ya kuiza au kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua kikaango cha ukubwa wa wastani chenye mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka vitunguu swaumu kwenye hicho kikaango, na ukaange kwa muda wa dakika 1, au hadi utakapo ona vitunguu swaumu vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step2

  Weka mbegu za shamari, mbegu za binzari nyembamba, mbegu za uwatu, mbegu za iliki, majani ya mbei pamoja na zafarani, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2. Epua mchanganyiko huo na uweke pembeni ili upoe.

  Step3

  Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga mchanganyiko ulio ukaanga, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vizuri. Ondoa mchanganyiko ulio usaga kutoka kwenye mashine ya kusaga, na uweke kwenye kontena safi.

  Step4

  Weka kwenye hilo kontena, tangawizi, mdalasini, karafuu, basibasi, pamoja na kungumanga, kisha changanya vizuri.

  Step5

  Hifadhi mchanganyiko huo kwenye chombo chenye mfuniko na kutumia kidogo kidogo kwenye mapishi yako.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *