Jarida la Mapishi

Achari ya kijani

Achari ya kijani | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    -
  • Walaji
    1

Achari ya kijani, ni achari rahisi kutengeneza ambayo hutengenezwa kwa kutumia mimea yenye rangi ya kijani kama vile majani ya minti na majani ya giligilani. Achari hii yafaa kutumika kwenye vitafunio kama vile sandwich. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza achari hii ya kijani.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka vitunguu vya kijani kwenye hiyo mashine ya kusaga, kisha saga hadi utakapo ona vitunguu hivyo vimesagika vyema na kuwa laini.

    Step2

    Weka majani ya minti pamoja na majani ya giligilani, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.

    Step3

    Weka limao, chumvi, sukari, pamoja na pilipili manga, kisha endelea kusaga hadi utakapo ona mchanganyiko huo wote umechanganyika vizuri.

    Step4

    Ondoa mchanganyiko huo kutoka kwenye mashine ya kusaga, kisha uhifadhi kwenye chombo chenye mfuniko na kutumia kidogo kidogo kwenye chakula cha aina yoyote ile.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.