-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 5
-
Walaji1
Ingredients
Directions
Chukua kikaango kidogo na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kikaango kipate moto. Weka dengu kwenye hicho kikaango, halafu kaanga bila kutumia mafuta huku ukikoroga na kutikisa kikaango mara kwa mara kwa muda wa dakika 1 mpaka 2, au hadi utakapo ona zimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia, kisha epua na uweke pembeni ili zipoe.
Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka dengu ulizo zikaanga kwenye hiyo mashine ya kusaga, kisha saga hadi utakapo ona dengu hizo zimesagika vizuri. Ondoa dengu hizo kwenye mashine ya kusaga na uziweke pembeni kwenye kontena.
Weka kwenye hiyo hiyo mashine ya kusaga, majani ya giligilani, vitunguu swaumu, pamoja na limao, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.
Weka dengu zilizomo kwenye kontena pamoja na chumvi, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo wote umechanganyika vizuri.
Weka achari hiyo kwenye chombo safi chenye mfuniko, kisha hifadhi kwenye friji.
Leave a Review