![Samaki wa kuoka | Jarida la Mapishi](https://www.jaridalamapishi.co.tz/wp-content/uploads/2023/11/samaki_wa_kuoka.jpg)
-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 10
-
Walaji4
Samaki wa kuoka, ni kitoweo kitamu na rahisi kupika, ambacho huandaliwa kwa kutumia minofu ya samaki wabichi walio changanywa na viungo, kisha kuokwa kwenye jiko la kuokea (oven). Waweza kula kitoweo hiki cha samaki wa kuoka kama chakula cha mchana au cha jioni, pamoja na wali au tambi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika kitoweo hiki cha samaki wa kuoka.
Ingredients
Directions
Chukua kontena kubwa. Weka ndani ya hilo kontena, binzari ya manjano pamoja na chumvi, kisha changanya vizuri.
Weka minofu ya samaki, kisha changanya vizuri hadi utakapo ona minofu yote ya samaki imeenea vyema binzari ya manjano na chumvi. Funika vizuri kontena hilo, kisha liweke kwenye friji kwa muda wa saa 1 mpaka saa 24.
Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, tangawizi, vitunguu swaumu, mafuta ya kupikia, heavy cream, limao, mbegu za haradali, pamoja na mbegu za kisibiti, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vizuri.
Weka mchanganyiko huo ulio usaga kwenye kontena lenye samaki, kisha changanga vizuri hadi utakapo ona minofu yote ya samaki imeenea vyema viungo. Funika vizuri kontena hilo, kisha liweke tena kwenye friji kwa muda wa saa 1.
Washa upande chini wa jiko la kuoka (oven) na uweke joto la nyuzi 190° C, kisha acha jiko lipate moto. Chukua sinia la kuokea na ulipake mafuta, kisha weka minofu ya samaki kwenye hilo sinia.
Weka sinia hilo ndani ya jiko la kuoka na uoke kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona upande huo wa chini wa minofu hiyo umebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.
Geuza upande wa pili wa minofu hiyo ya samaki, kisha endelea kuoka kwa muda wa dakika 4 mpaka 5, au hadi utakapo ona na upande huo wa pili wa minofu hiyo umebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.
Ondoa minofu hiyo ya samaki kutoka kwenye jiko la kuoka na uweke kwenye sahani, tayari kwa kula.
Leave a Review