-
MaandaliziDakika 30
-
KupikaDakika 20
-
Walaji4
Wali wa viungo, ni chakula kitamu na rahisi kupika, ambacho hupikwa kwa kutumia viungo vya aina mbalimbali kama vile, zafarani na binzari nyembamba. Wali huu wafaaa kula pamoja na mchuzi wa nyama au au mchuzi wa kuku. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika wali huu wa viungo.
Ingredients
Directions
Chukua kontena la ukubwa wa wastani. Weka maji, kisha roweka mchele ndani ya hilo kontena lenye maji kwa muda wa dakika 30. Baada ya dakika 30, ondoa mchele kwenye kontena na uweke pembeni kwenye chombo safi, kisha ukaushe vizuri.
Chukua sufuria la ukubwa wa wastani na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha sufuria lipate moto. Weka kwenye hilo sufuria, binzari nyembamba, pilipili manga, zafarani, pamoja na iliki, kisha kaanga bila kutumia mafuta huku ukikoroga na kutikisa kikaango mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.
Weka mchele ulio ukausha, kisha kaanga huku ukiugeuza na kutikisa kikaango mara kwa mara kwa muda wa dakika 2 mpaka 3.
Weka maji uliyotumia kurowekea mchele pamoja na chumvi, halafu koroga vizuri, kisha weka moto mkubwa na uache ichemke.
Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka taratibu kwa muda wa dakika 10 mpaka 15, au hadi utakapo ona wali umeiva na maji yote kwenye sufuria yamekauka. Hakikisha hukorogi kabisa wali wakati unaupika.
Zima jiko, kisha acha wali utulie kwa muda wa dakika 5, ukiwa bado juu ya jiko. Baada ya dakika 5, pakua wali kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Leave a Review