Jarida la Mapishi

Mchuzi wa mayai

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 45
 • Walaji
  4

Mchuzi wa mayai, ni chakula kitamu ambacho unaweza kukipika kwa muda mfupi wa ndani ya dakika 30 tu. Chakula hiki hupikwa kwa kutumia mayai yaliyo chemshwa, nyanya, pamoja na viungo. Unaweza kula chakula hiki pamoja na wali au chapati. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mchuzi huu wa mayai.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua sufuria la ukubwa wa wastani. Weka kwenye hilo sufuria maya 6 pamoja na maji kiasi, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa.

  Step2

  Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 10 mpaka 12, au hadi utakapo ona mayai yameiva. Epua na uweke pembeni ili ipoe.

  Step3

  Menya maganda ya mayai hayo, kisha yakate katikati.

  Step4

  Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, nazi iliyokunwa, vitunguu swaumu, mbegu za giligilani, mbegu za haradali, binzari nyembamba, binzari ya manjano pamoja na star anise, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vyema na kuwa laini.

  Step5

  Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka vitunguu maji kwenye hilo sufuria, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona vimeiva.

  Step6

  Weka mchanganyiko wa nazi ulio usaga, kisha endelea kukaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5 zaidi.

  Step7

  Weka vikombe 3 vya maji, Tamarind Paste, pamoja na chumvi, halafu koroga vizuri,kisha weka moto mkubwa na uache ichemke.

  Step8

  Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 15, au hadi utakapo ona mchuzi umekuwa laini.

  Step9

  Mimina tui la nazi halafu koroga vizuri, kisha acha ichemke.

  Step10

  Chukua kontena dogo. Weka ndani ya hilo kontena, vijiko vya chakula vya tui la nazi, pamoja na mayai yaliyobaki, kisha changanya kwa kupiga piga vizuri mchanganyiko huo.

  Step11

  Mimina mchanganyiko huo wa mayai kwenye sufuria lenye mchuzi, kisha koroga kwa muda wa dakika 2.

  Step12

  Weka mayai uliyo yachemsha, halafu acha ichemke kwa muda wa dakika 5, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *