Jarida la Mapishi

Pilau ya giligilani

 • Maandalizi
  Dakika 30
 • Kupika
  Dakika 25
 • Walaji
  4

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua kontena la ukubwa wa wastani. Weka maji, kisha roweka mchele ndani ya hilo kontena lenye maji kwa muda wa dakika 30.

  Step2

  Chukua sufuria la ukubwa wa wastani lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, binzari nyembamba, mdalasini, iliki, pamoja na vitunguu maji kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 3, au hadi utakapo ona vitunguu vimeiva.

  Step3

  Weka vitunguu swaumu, njegere, majani ya giligilani, garam masala, pamoja na chumvi, kisha endelea kukaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2 zaidi.

  Step4

  Weka mchele pamoja na maji uliyotumia kurowekea mchele, halafu koroga vizuri, kisha weka moto mkubwa na uache ichemke.

  Step5

  Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka taratibu kwa muda wa dakika 10 mpaka 15, au hadi utakapo ona wali umeiva na maji yote kwenye sufuria yamekauka. Hakikisha hukorogi kabisa wali wakati unaupika.

  Step6

  Wali ukishaiva zima jiko na uache utulie kwa muda wa dakika 5, ukiwa bado juu ya jiko. Baada ya dakika 5, pakua pilau kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *