Jarida la Mapishi

Kuku wa binzari nyembamba na pilipili hoho

Kuku wa binzari nyembamba na pilipili hoho | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 15
  • Walaji
    4

Kuku wa binzari nyembamba na pilipili hoho, ni kitoweo kitamu kinachopikwa kwa kutumia nyama ya kuku, pilipili hoho, pamoja na viungo mbalimbali kama vile, binzari nyembamba, binzari ya manjano, nyanya, pamoja vitunguu. Kitoweo hiki chafaa kula kwenye sherehe za aina mbalimbali. Pia waweza kula kitoweo hiki pamoja na mkate. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika kitoweo hiki cha kuku wa binzari nyembamba na pilipili hoho.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kontena kubwa. Weka ndani ya hilo kontena, vipande vya nyama ya kuku, tangawizi, vitunguu swaumu, white vinegar, pilipili manga, pamoja na chumvi, kisha changanya vizuri hadi utakapo ona vipande vyote vya nyama ya kuku vimechanganyika vyema pamoja na viungo.

    Step2

    Funika vizuri kontena hilo, kisha liweke kwenye friji kwa muda wa saa 4 mpaka 24.

    Step3

    Chukua sufuria la ukubwa wa wastani lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, binzari nyembamba, vipande vya nyama ya kuku pamoja na mchanganyiko wake wote wa viungo, kisha pika mchanganyiko huo huku ukivigeuza vipande hivyo vya nyama ya kuku mara kwa mara kwa muda wa dakika 7, au hadi utakapo ona pande zote za vipande hivyo vya nyama ya kuku vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step4

    Mimina mtindi taratibu huku ukikoroga. Weka vitunguu maji pamoja na pilipili hoho, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona nyama ya kuku imekuwa laini na mchuzi umekauka.

    Step5

    Weka majani ya giligiliani, kisha endelea kupika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1 zaidi.

    Step6

    Nyunyizia garam masala na ukoroge vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Conclusion

    Kabla ya kutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.