Jarida la Mapishi

Mishikaki ya kuku wa kusaga

 • Maandalizi
  Saa 4
 • Kupika
  Dakika 10
 • Walaji
  4

Mishikaki ya kuku wa kusaga, ni mishikaki mitamu na rahisi kupika. Mishikaki hii huandaliwa kwa kuchanganya nyama ya kuku wa kusaga pamoja na viungo. Unaweza kuipika mishikaki hii kwa kuichoma kwenye jiko la kuchomea nyama au kwa kuioka kwenye jiko la kuokea (oven). Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mishikaki hii ya kuku.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua kontena dogo. Weka ndani ya hilo kontena, limao, siagi, pamoja na Chaat Masala halafu changanya vizuri, kisha weka pembeni.

  Step2

  Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, vipande vya nyama ya kuku, vitunguu maji, korosho, vitunguu swaumu, tangawizi, ute wa mayai, kungumanga, pilipili nyeupe, mbegu za giligilani, pamoja na garam masala, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini. Ondoa mchanganyiko huo kutoka kwenye mashine ya kusaga na uweke kwenye kontena.

  Step3

  Funika kontena hilo vizuri, kisha liweke kwenye friji kwa muda wa saa 4.

  Step4

  Chukua kontena la ukubwa wa wastani. Weka maji, kisha roweka vijiti vya mishikaki ndani ya hilo kontena lenye maji kwa muda wa dakika 30.

  Step5

  Baada ya dakika 30, mwaga maji yote yaliyomo kwenye kontena na kubakiwa na vijiti peke yake.

  Step6

  Ondoa kontena lenye mchanganyiko wa nyama ya kuku kwenye friji na uliweke pembeni. Lowanisha vidole vyako na maji, halafu weka unga wa ngano ndani ya hilo kontena, kisha changanya vizuri.

  Step7

  Gawa mchanganyiko huo wa nyama ya kuku katika mafungu 15 yenye uwiano sawa. Chukua fungu moja na uviringishe vizuri, ili kutengeneza umbo refu na nene kama soseji. Rudia hatua hii kwa mafungu mengine ya mchanganyiko wa nyama ya kuku yaliyobaki.

  Step8

  Chukua vijiti vya mishikaki. Chomeka mchanganyiko wa nyama ya kuku ulio viringisha katika umbo la soseji kwenye hivyo vijiti vya mishikaki, kisha paka juu ya hiyo mishikaki mchanganyiko wa siagi ulio changanya mwanzoni.

  Step9

  Washa jiko la kuchomea nyama, kisha acha jiko lipate moto. Weka mishikaki juu ya jiko la kuchomea nyama, kisha choma mishikaki hiyo huku ukigeuza mara kwa mara kwa muda wa dakika 10, au hadi utakapo ona pande zote za mishikaki hiyo zimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step10

  Ondoa mishikaki hiyo kwenye jiko la kuchomea nyama na uiweke kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *