Jarida la Mapishi

Saladi ya viazi vitamu

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 20
 • Walaji
  4

Saladi ya viazi vitamu, ni saladi ambayo asili yake ni kutoka katika mataifa ya Kiarabu. Saladi hii hutengenezwa kwa kutumia viazi vitamu, Tamarind Paste pamoja na viungo. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza saladi hii ya viazi vitamu.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua kikaango kidogo na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kikaango kipate moto. Weka kwenye hicho kikaango mbegu za binzari nyembamba, halafu kaanga bila kutumia mafuta huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa sekunde 30, kisha epua na uweke pembeni ili zipoe.

  Step2

  Chukua kinu. Weka ndani ya hicho kinu mbegu za binzari nyembamba ulizo zikaanga, kisha twanga hadi utakapo ona mbegu hizo zimesagika vizuri.

  Step3

  Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria viazi vitamu pamoja na maji, kisha chemsha kwenye jiko lenye moto wa wastani kwa muda wa dakika 15, au hadi utakapo ona vimeiva. Epua viazi hivyo na uviweke pembeni ili vipoe. Viazi vikishapoa, vimenye maganda yake yote, kisha vikate katika vipande vidogo vidogo.

  Step4

  Chukua kontena kubwa. Weka ndani ya hilo kontena viazi vitamu, majani ya giligilani, chumvi, brown sugar, tangawizi, binzari nyembamba, pamoja na Tamarind Paste, changanya vizuri. Funika kontena vizuri, kisha weka saladi kwenye friji kwa muda wa saa 1 kabla ya kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *