Jarida la Mapishi

Saladi ya karoti na korosho

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 5
 • Walaji
  4

Saladi ya karoti na korosho, ni saladi nzuri, yenye afya na rahisi sana kutengeneza, ambayo hutengenezwa kwa kutumia karoti mbichi ambazo huchanganywa pamoja na korosho na viungo. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza saladi hii ya karoti na korosho.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua kontena kubwa. Weka ndani ya hilo kontena, karoti, nazi, korosho, majani ya giligilani, chumvi, pamoja na limao, kisha changanya vizuri.

  Step2

  Chukua sufuria dogo lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, mbegu za haradali, binzari nyembamba, pamoja na majani ya mvuje, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1. Epua mchanganyiko huu na umimine kwenye kontena lenye mchanganyiko wa karoti, kisha changanya vizuri, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *