Jarida la Mapishi

Saladi ya karanga

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 5
 • Walaji
  4

Saladi ya karanga, ni saladi ambayo hutengenezwa kwa kutumia karanga zilizo kaangwa bila mafuta, juisi ya machungwa, nyanya, limao, vitunguu vya kijani pamoja na viungo. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza saladi hii ya karanga.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua kontena la ukubwa wa wastani. Weka ndani ya hilo kontena, juisi ya machungwa, kijiko 1 cha chai cha Chaat Masala, majani ya minti, chumvi, pamoja na karanga, kisha changanya vizuri.

  Step2

  Funika kontena hilo vizuri, kisha liweke kwenye friji kwa muda wa saa 2 mpaka 4.

  Step3

  Chukua kikaango kikubwa na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kikaango kipate moto. Weka kwenye hicho kikaango mchanganyiko wa karanga uliomo kwenye kontena, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara, hadi utakapo ona maji maji yote yamekauka. Epua mchanganyiko huu na uweke kwenye kontena jingine, kisha acha ipoe.

  Step4

  Weka kwenye hilo kontena, nyanya, vitunguuu vya kijani, majani ya giligilani, limao, pamoja na kijiko 1 cha chai cha Chaat Masala kilichobaki, kisha changanya vizuri, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *