-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 5
-
Walaji4
Saladi ya kabichi na kitunguu, ni saladi ambayo sio tu ni rahisi kutengeneza, bali pia ni tamu. Saladi hii ya kabichi na kitunguu yafaa kuliwa pamoja na chakula chochote kile ukipendacho au nyama choma. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza saladi hii ya kabichi na kitunguu.
Ingredients
Directions
Chukua kikaango kidogo na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kikaango kipate moto. Weka mbegu za ufuta kwenye hicho kikaango, halafu kaanga bila kutumia mafuta huku ukikoroga na kutikisa kikaango mara kwa mara kwa muda wa sekunde 30, kisha epua na uweke pembeni ili ipoe.
Chukua kontena kubwa. Weka ndani ya hilo kontena, vitunguu maji, kabichi, pilipili hoho, pamoja na nyanya, kisha changanya vizuri.
Chukua sufuria dogo lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, mbegu za haradali pamoja na majani ya mvuje, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa sekunde 30.
Weka white vinegar pamoja na chumvi, kisha koroga vizuri. Epua mchanganyiko huu na umimine kwenye kontena lenye saladi.
Nyunyizia mbegu za ufuta, kisha changanya vizuri.
Funika vizuri kontena hilo lenye saladi, kisha liweke kwenye friji kwa muda wa saa 2, kabla ya kula.
Leave a Review