Jarida la Mapishi

Saladi ya maharage ya soya

Saladi ya maharage ya soya | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 10
  • Walaji
    4

Saladi ya maharage ya soya, ni saladi nzuri ambayo hutengenezwa kwa kutumia maharage ya soya yaliyo chemshwa, mboga ya mchunga, nyanya, vitunguu vya kijani, pamoja na viungo. Saladi hii yafaa sana kula pamoja na nyama choma. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza saladi hii ya maharage.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kontena kubwa. Weka ndani ya hilo kontena, mboga ya mchunga, nyanya, pamoja na vitunguu vya kijani, kisha changanya vizuri.

    Step2

    Chukua sufuria la ukubwa wa wastani lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, tangawizi, binzari nyembamba, vitunguu swaumu, mbegu za giligilani, pilipili manga, maharage ya soya, ½ kikombe cha maji uliyotumia kuchemshia maharage ya soya, pamoja na chumvi, halafu koroga vizuri, kisha funika sufura na upike mchanganyiko huo huku ukikoroga na kutikisa sufuria mara kwa mara kwa muda wa dakika 5. Epua mchanganyiko huu na umimine kwenye kontena lenye mchanganyiko wa mboga ya mchunga.

    Step3

    Weka limao pamoja na Chaat Masala, kisha changanya vizuri, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.