-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 15
-
Walaji4
Saladi ya magimbi, ni saladi tamu ambayo hutengenezwa kwa kwa kutumia magimbi yaliyo chemshwa, majani ya minti, limao, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza saladi hii ya magimbi.
Ingredients
Directions
Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria magimbi pamoja na maji, kisha chemsha kwenye jiko lenye moto wa wastani kwa muda wa dakika 15, au hadi utakapo ona yameiva.
Epua na umwage maji yote yaliyomo kwenye sufuria na kubakiwa na magimbi peke yake, kisha acha yapoe.
Menya maganda ya magimbi hayo, kisha yakate katika vipande vidogo vidogo.
Chukua kontena. Weka ndani ya hilo kontena, magimbi uliyo yachemsha, chumvi, mbegu za kisibiti, Chaat Masala, majani ya minti, limao, pamoja na majani ya giligilani, kisha changanya vizuri, tayari kwa kula.
Leave a Review