Jarida la Mapishi

Mchuzi wa kamba

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 40
 • Walaji
  4

Mchuzi wa kamba, ni kitoweo kitamu na rahisi kupika, ambacho hupikwa kwa kutumia kamba wabichi, nyanya, vitunguu maji, pamoja na viungo. Mchuzi huu wa kamba, wafaa kula pamoja na wali au chapati. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mchuzi huu wa kamba.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, vitunguu swaumu, tangawizi, majani ya mvuje, binzari nyembamba, mbegu za haradali, garam masala, chumvi, sukari, binzari ya manjano, pamoja na white vinegar, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri. Ondoa mchanganyiko huo kutoka kwenye mashine ya kusaga, na uweke pembeni kwenye kontena.

  Step2

  Weka nyanya kwenye hiyo hiyo mashine ya kusaga, kisha saga hadi utakapo ona nyanya hizo zimesagika vizuri na kuwa laini.

  Step3

  Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria mdalasini pamoja na majani ya mbei, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa sekunde 30.

  Step4

  Weka vitunguu maji, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 7, au hadi utakapo ona vitunguu maji vimeiva.

  Step5

  Weka mchanganyiko ulio usaga, kisha pika mchanganyiko huo katika moto mdogo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 10, au hadi utakapo ona mchanganyiko huo umebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step6

  Weka nyanya ulizo zisaga, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 10, au hadi utakapo ona mchuzi umekuwa mzito.

  Step7

  Weka kamba kisha endelea kupika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 7, au hadi utakapo ona kamba wamebadilika rangi na kuwa na rangi ya pinki.

  Step8

  Weka majani ya giligilani na ukoroge vizuri, halafu acha ichemke kwa muda wa dakika 2, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *