Jarida la Mapishi

Mchuzi wa nyama ya ng’ombe

Mchuzi wa nyama ya ng’ombe | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Saa 1 Dk. 55
  • Walaji
    4

Mchuzi wa nyama ya ng’ombe, ni kitoweo chenye ladha na harufu nzuri. Kitoweo hiki hupikwa kwa kutumia nyama ya ng’ombe, vitunguu maji, nyanya, mtindi, pamoja na viungo. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mchuzi huu wa nyama ya ng’ombe.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto mkubwa, kisha acha mafuta yapate moto. Weka vitunguu maji kwenye hilo sufuria, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 3 mpaka 5.

    Step2

    Punguza moto na uweke moto mdogo, kisha endelea kukaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 12, au hadi utakapo ona vitunguu vimeiva.

    Step3

    Weka tangawizi pamoja na vitunguu swaumu, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.

    Step4

    Weka nyanya, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona mchuzi umekuwa mzito.

    Step5

    Weka mbegu za giligilani, garam masala, binzari nyembamba, pamoja na binzari ya manjano, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa sekunde 30.

    Step6

    Weka nyama ya ng'ombe pamoja na chumvi, halafu ongeza moto na uweke moto mkubwa, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 3 mpaka 5.

    Step7

    Punguza moto na uweke moto mdogo, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 15 mpaka 20, au hadi utakapo ona nyama imebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step8

    Minina mtindi taratibu huku ukikoroga, kisha endelea kupika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5.

    Step9

    Mimina maji halafu koroga vizuri, kisha funika sufuria na uache ichemke kwa muda wa dakika 45 mpaka 55, au hadi utakapo ona nyama imeiva na mchuzi umekuwa mzito.

    Step10

    Weka majani ya uwatu na ukoroge vizuri, halafu iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 5 zaidi, kisha epua na upakue kwenye safi, tayari kwa kula.

    Conclusion

    Kabla ya kutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.