Jarida la Mapishi

Mchuzi wa nguruwe

Mchuzi wa nguruwe | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Saa 1 Dk. 10
  • Walaji
    4

Mchuzi wa nguruwe, ni pishi rahisi sana kupika ambalo hupikwa kwa kutumia nyama ya nguruwe pamoja viungo. Pishi hili lafaa kuliwa pamoja na chakula chochote kile upendacho hasa chakula cha wakati wa jioni, iwe wali, ugali au chakula kingine chochote upendacho. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mchuzi huu wa nguruwe.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kikaango kidogo na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kikaango kipate moto. Weka kwenye hicho kikaango, mbegu za giligilani, mbegu za binzari nyembamba, mbegu za haradali, pamoja na mbegu za pilipili manga, halafu kaanga huku ukikoroga na kutikisa kikaango mara kwa mara kwa muda wa dakika 2, kisha epua na uweke pembeni ili ipoe.

    Step2

    Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka mchanganyiko wa viungo ulio kaanga kwenye hiyo mashine ya kusaga, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini. Ondoa mchanganyiko huo kutoka kwenye mashine ya kusaga, na uweke pembeni kwenye kontena. Weka binzari ya manjano, mdalasini, kungumanga, pamoja na chumvi, kisha changanya vizuri.

    Step3

    Weka kwenye hiyo hiyo mashine ya kusaga, ½ ya vitunguu maji ulivyo vikata, tangawizi, vitunguu swaumu, tui la nazi, pamoja na Tamarind Paste, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vyema na kuwa laini. Mimina mchanganyiko wa viungo uliomo kwenye kontena, kisha saga tena hadi utakapo ona mchanganyiko huo wote umechanganyika vizuri.

    Step4

    Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka ½ ya vitunguu maji vilivyobaki kwenye hilo sufuria, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 10, au hadi utakapo ona vitunguu vimeiva.

    Step5

    Weka mchanganyiko ulio usaga, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 10, au hadi utakapo ona mchanganyiko huo umebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step6

    Weka nyama ya nguruwe, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 15, au hadi utakapo ona nyama imebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step7

    Mimina maji halafu koroga vizuri, kisha weka moto mkubwa na uache ichemke.

    Step8

    Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wastani, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 30, au hadi utakapo ona nyama imeiva na mchuzi umekuwa mzito. Epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.