Jarida la Mapishi

Biriani ya mboga

 • Maandalizi
  Dakika 30
 • Kupika
  Dakika 50
 • Walaji
  4

Biriani ya mboga, ni chakula kitamu na chenye harufu nzuri ambacho hupikwa kwa kutumia mchele, mboga mchanganyiko, pamoja na viungo. Biriani hii ya mboga kama zilizvyo biriani nyingine zote, ni chakula ambacho chafaa kuliwa kwenye sherehe au sikukuu. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika biriani hii ya mboga.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua kikombe chenye maziwa, kisha roweka zafarani ndani ya hicho kikombe chenye maziwa kwa muda wa dakika 30.

  Step2

  Chukua kikaango kidogo na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kikaango kipate moto. Weka mchanganyiko wa njugu kwenye hicho kikaango, halafu kaanga bila kutumia mafuta huku ukikoroga na kutikisa kikaango mara kwa mara kwa muda wa dakika 3, au hadi utakapo ona zimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia, kisha epua na uweke pembeni.

  Step3

  Chukua sufuria kubwa lenye siagi na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha siagi iyeyuke. Weka kwenye hilo sufuria, mdalasini, karafuu, iliki, pamoja na majani ya mbei, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.

  Step4

  Weka vitunguu maji, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 7, au hadi utakapo ona vitunguu maji vimeiva.

  Step5

  Weka tangawizi pamoja na vitunguu swaumu, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.

  Step6

  Weka mchanganyiko wa mboga, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5 mpaka 7.

  Step7

  Mimina mtindi taratibu huku ukikoroga, halafu acha ichemke kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona mtindi umekaribia kukauka, kisha epua na uweke pembeni.

  Step8

  Washa jiko la kuoka na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto.

  Step9

  Chukua sufuria jingine kubwa. Mimina mchuzi wa mboga mchanganyiko uliyoipika kwenye hilo sufuria.

  Step10

  Weka nusu ya wali mweupe uliopikwa juu ya huo mchuzi, kisha sambaza vizuri.

  Step11

  Weka mchanganyiko wa mboga ulioupika juu ya huo wali, kisha sambaza vizuri.

  Step12

  Nyunzia limao, majani ya giligilani, pamoja na majani ya minti, juu ya huo mchanganyiko wa mboga.

  Step13

  Weka nusu ya wali uliobaki, kisha sambaza vizuri.

  Step14

  Nyunyizia maziwa yenye zafarani juu ya huo wali, kisha funika vizuri sufuria hilo kwa kutumia aluminium foil.

  Step15

  Weka sufuria hilo ndani ya jiko la kuoka, kisha oka kwa muda wa dakika 30, au hadi utakapo ona biriani imeiva. Ondoa sufuria hilo kwenye jiko la kuoka na uliweke pembeni.

  Step16

  Weka mchanganyiko wa njugu ulizo zikaanga kwenye hilo sufuria lenye biriani, kisha changanya vizuri, tayari kwa kula.

  Conclusion

  Kabla ya kutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *