Jarida la Mapishi

Pilau ya mboga

Pilau ya mboga | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 30
  • Walaji
    4

Pilau ya mboga, ni pilau ambayo hupikwa kwa kutumia mchele, mchanganyiko wa mboga mbali mbali, pamoja na viungo kama vile, binzari nyembamba na karafuu. Kuna namna nyingi za kupika pilau hii, ila hapo chini tume ainisha njia bora na rahisi zaidi ya kupika pilau hii. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika pilau hii ya mboga.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, binzari nyembamba, karafuu, mbegu za shamari, majani ya mbei, pamoja na viazi mviringo, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2, au hadi utakapo ona vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step2

    Weka mchele, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 3.

    Step3

    Weka karoti, kauliflawa, pamoja na njegere, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika kadhaa.

    Step4

    Weka nyanya, mbegu za giligilani, garam masala, binzari ya manjano, pamoja na chumvi, kisha endelea kupika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 3 mpaka 5 zaidi.

    Step5

    Mimina maji halafu koroga vizuri, kisha weka moto mkubwa na uache ichemke.

    Step6

    Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka taratibu kwa muda wa dakika 10 mpaka 15, au hadi utakapo ona wali umeiva na maji yote kwenye sufuria yamekauka. Hakikisha hukorogi kabisa wali wakati unaupika.

    Step7

    Zima jiko. Weka majani ya giligilani halafu koroga vizuri, kisha acha pilau itulie kwa muda wa dakika 5, ikiwa bado juu ya jiko. Baada ya dakika 5, pakua pilau kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.