Jarida la Mapishi

Mishikaki ya mapaja ya kuku

Mishikaki ya mapaja ya kuku | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 20
  • Walaji
    4

Mishikaki ya mapaja ya kuku, ni mishikaki inayopikwa kwa kutumia nyama ya mapaja ya kuku, viungo, pamoja na mtindi. Watu wengine hutumia krimu katika pishi hili badala ya mtindi. Unaweza kupika mishikaki hii kwa kutumia jiko la kuchomea nyama au hata kwa kutumia jiko la kuoka (oven). Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mishikaki hii ya mapaja ya kuku.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kisu. Chanja mara 2 hadi 3 kwenye kila paja la kuku kwa kutumia ncha ya kisu, kisha weka mapaja hayo kwenye kontena kubwa.

    Step2

    Chukua bakuli ndogo. Weka ndani ya hilo bakuli, kungumanga, binzari ya manjano, mbegu za giligilani, 1 kijiko cha chai cha binzari nyembamba, majani ya uwatu, garam masala, tangawizi, vitunguu swaumu, limao, pamoja na mafuta ya kupikia, kisha changanya vizuri.

    Step3

    Mimina mchanganyiko huo kwenye kontena lenye mapaja ya kuku, kisha changanya vizuri hadi utakapo ona mapaja yote ya kuku yameenea vyema viungo.

    Step4

    Funika kontena hilo vizuri, kisha liweke kwenye friji kwa muda wa saa 8 mpaka saa 24.

    Step5

    Chukua kikaango kidogo chenye siagi na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha siagi ipate moto. Weka kijiko 1 cha chai cha binzari nyembamba kwenye hicho kikaango, halafu kaaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa sekunde kadhaa, kisha epua na uweke pembeni.

    Step6

    Chukua aluminium foil. Gawa aluminium foil hilo katika vipande vidogo vidogo, kisha tumia vipande hivyo kufunika kwenye mifupa ya mapaja ya kuku.

    Step7

    Washa jiko la kuchomea nyama, kisha acha jiko lipate moto. Weka mapaja ya kuku juu ya jiko la kuchomea nyama, kisha choma mapaja hayo huku ukiyageuza mara kwa mara kwa muda wa dakika 17 mpaka 18, au hadi utakapo ona pande zote za mapaja hayo zimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step8

    Paka mchanganyiko wa siagi kwenye mapaja hayo ya kuku, halafu endelea kuchoma kwa muda wa dakika 2 mpaka 3 zaidi, kisha ondoa kwenye jiko la kuchomea nyama na uweke kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.