Jarida la Mapishi

Kuku wa ukwaju

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 30
 • Walaji
  4

Kuku wa ukwaju, ni chakula kitamu na rahisi kupika chenye ladha ya mchanganyiko wa utamu na uchachu. Chakuka hiki chafaa sana kula pamoja na wali au tambi hasa katika msimu wa sikukuu. Fuata hatua zifuatazo,ili ujifinze jinsi ya kupika kuku huyu wa ukwaju.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, mdalasini, iliki, binzari nyembamba, pamoja na vitunguu maji, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 10, au hadi utakapo ona vitunguu maji vimeiva.

  Step2

  Weka tangawizi, vitunguu swaumu, vipande vya nyama ya kuku, mbegu za giligilani, binzari ya manjano, pamoja na chumvi, kisha kaanga huku ukikoroga na kuvigeuza vipande vya nyama ya kuku mara kwa mara kwa muda wa dakika 5 mpaka 7, au hadi utakapo ona vipande hivyo vya nyama ya kuku vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step3

  Weka Tamarind Paste, white vinegar, pamoja na brown sugar, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 8 mpaka 10, au hadi utakapo ona vipande vya nyama ya kuku vimeiva. Epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *