Jarida la Mapishi

Achari ya minti na nazi

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 1
 • Walaji
  1

Achari ya minti na nazi, ni achari yenye ladha nzuri ambayo hutengenezwa kwa kutumia majani mabichi ya minti, nazi iliyokunwa, pamoja na viungo vya aina mbali mbali kama vile vitunguu swaumu na binzari nyembamba. Achari hii yafaa kutumia kaka kifungua kinywa wakati wa asubuhi pamoja na vitafunio vya aina mbali mbali kama vile, sambusa, sandwich au chapati. Pia waweza kutumia achari hii kwenye mishikaki. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza achari hii ya minti na nazi.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua kikaango kidogo na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kikaango kipate moto. Weka mbegu za binzari myembamba manga kwenye hicho kikaango, halafu kaanga bila kutumia mafuta huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa sekunde 30, kisha epua na uweke pembeni ili ipoe.

  Step2

  Chukua kinu. Weka ndani ya hicho kinu mbegu za binzari nyembamba ulizo zikaanga, kisha twanga hadi utakapo ona mbegu hizo zimesagika vizuri.

  Step3

  Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, nazi, tangawizi, pamoja na vitunguu swaumu, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.

  Step4

  Weka majani ya giligilani, majani ya minti, Tamarind Paste, binzari nyembamba, pamoja na chumvi, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo wote umesagika vyema na kuwa laini.

  Step5

  Ondoa mchanganyiko huo kutoka kwenye mashine ya kusaga, kisha uhifadhi kwenye chombo chenye mfuniko na kutumia kidogo kidogo kwenye chakula cha aina yoyote ile.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *