Jarida la Mapishi

Wali wa limao

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 20
 • Walaji
  4

Wali wa limao, ni wali rahisi sana kuupika ambao unaweza kuupika kwa haraka. Chakula hiki, hupikwa kwa kutumia wali uliokwisha pikwa, viungo, pamoja na karanga. Fuata hatua zifuatazo, ili uweze kujifunza jinsi ya kupika wali huu wa limao.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua sufuria la ukubwa wa wastani. Weka kwenye hilo sufuria, mchele, maji, binzari ya manjano, pamoja na chumvi, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa.

  Step2

  Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka taratibu kwa muda wa dakika 12 mpaka 15, au hadi utakapo ona wali umeiva na maji yote kwenye sufuria yamekauka. Hakikisha hukorogi kabisa wali wakati unaupika.

  Step3

  Weka limao halafu koroga vizuri, kisha epua na upakue kwenye kontena. Funika vizuri kontena hilo, kisha weka pembeni.

  Step4

  Chukua sufuria dogo lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, choroko, dengu, mdalasini, pamoja karafuu, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1, au hadi utakapo ona choroko na dengu vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step5

  Weka mbegu za haradali, majani ya giligilani, pamoja na majani ya mvuje, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1 zaidi. Epua mchanganyiko huu na umimine kwenye kontena lenye wali, kisha changanya vizuri, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *