Jarida la Mapishi

Achari ya giligilani

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  -
 • Walaji
  1

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua sufuria ndogo lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria mbegu za haradali pamoja na mbaazi, kisha kaanga huku ukitikisa sufuria kwa muda wa dakika 1, au hadi utakapo ona mbaazi zimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia. Epua mchanganyiko huu na uweke pembeni ili upoe.

  Step2

  Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka mchanganyiko ulio ukaanga kwenye hiyo mashine ya kusaga, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.

  Step3

  Weka Tamarind Paste, chumvi, pamoja na majani ya giligilani, kisha endelea kusaga hadi utakapo ona mchanganyiko huo wote umesagika vyema na kuwa laini.

  Step4

  Ondoa mchanganyiko huo kutoka kwenye mashine ya kusaga, kisha uhifadhi kwenye chombo chenye mfuniko na kutumia kidogo kidogo kwenye chakula cha aina yoyote ile.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *