Jarida la Mapishi

Viungo vya nyama

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 10
 • Walaji
  1

Viungo vya nyama, ni mchanganyiko wa viungo, ambavyo hutumika kwenye mapishi ya aina mbalimbali ya nyama, kama vile nyama ya kuchoma, nyama ya mchuzi, au hata nyama ya kukaanga. Viungo hivi vya nyama ni kwa ajili ya nyama za aina zote, iwe ni nyama ya ng'ombe, nyama ya mbuzi, au nyama ya kondoo. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza viungo hivi vya nyama kwa ajili ya kuuza au kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua kikaango cha ukubwa wa wastani. Weka karanga kwenye hicho kikaango, kisha kaanga bila kuweka mafuta huku ukikoroga na kutikisa kikaango kwa muda wa dakika 1.

  Step2

  Weka dengu, mbegu za binzari nyembamba, pamoja na mbegu za uwatu, kisha kaanga kwa muda wa dakika 2 mpaka 3, au hadi utakapo ona viungo hivyo vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step3

  Weka mbegu za ufuta, mbegu za giligilani, mbegu za mpopi, pamoja na mbegu za haradali, halafu endelea kukaanga kwa muda wa dakika 2 mpaka 3 zaidi, kisha epua na uweke pembeni ili ipoe.

  Step4

  Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga mchanganyiko wa karanga na viungo ulio ukaanga, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri.

  Step5

  Ondoa mchanganyiko huo kutoka kwenye mashine ya kusaga, kisha uhifadhi kwenye chombo chenye mfuniko na kutumia kidogo kidogo kwenye mapishi yako ya nyama.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *