Jarida la Mapishi

Wali wa korosho

Wali wa korosho | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 20
  • Walaji
    4

Wali wa korosho, ni wali mtamu, wenye harufu nzuri sana na ambao pia ni rahisi sana kupika. Wali huu hupikwa kwa kutumia mchele, korosho mbichi, mtindi, matango, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika wali huu wa korosho.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua sufuria la ukubwa wa wastani. Weka kwenye hilo sufuria, mchele, maji, pamoja na chumvi halafu koroga vizuri, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa.

    Step2

    Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, halafu funika sufuria na uache iendelee kuchemka taratibu kwa muda wa dakika 12 mpaka 15, au hadi utakapo ona wali umeiva na maji yote kwenye sufuria yamekauka, kisha epua na uweke pembeni. Hakikisha hukorogi kabisa wali wakati unaupika.

    Step3

    Chukua kontena la ukubwa wa wastani. Weka ndani ya hilo kontena, mtindi, matango, pamoja na tangawizi, kisha changanya vizuri. Mimina mchanganyiko huu kwenye sufuria lenye wali halafu changanya vizuri, kisha funika sufuria.

    Step4

    Chukua sufuria dogo lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, mbegu za haradali, korosho, pamoja na majani ya mvuje, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2. Epua mchanganyiko huu na umimine kwenye sufuria lenye mchanganyiko wa wali, kisha changanya vizuri, tayari kwa kula.

    Conclusion

    Kabla ya kutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.