Jarida la Mapishi

Viazi vya kuponda

Viazi vya kuponda | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 25
  • Walaji
    4

Viazi vya kuponda, ni chakula kitamu, rahisi kupika na chenye afya. Chakula hiki hupikwa kwa kutumia viazi mviringo vilivyo chemshwa, kisha kupondwa, vitunguu vya kijani, mtindi, pamoja na viungo. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika viazi hivi vya kuponda.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria viazi mviringo pamoja na maji, kisha chemsha kwenye jiko lenye moto wa wastani kwa muda wa dakika 20, au hadi utakapo ona vimeiva.

    Step2

    Epua na umwage maji yote yaliyomo kwenye sufuria na kubakiwa na viazi peke yake, kisha acha vipoe.

    Step3

    Menya maganda ya viazi hivyo, halafu vikate katika vipande vidogo vidogo, kisha viponde vizuri.

    Step4

    Chukua kontena. Weka ndani ya hilo kontena, viazi ulivyo viponda, mtindi, vitunguu vya kijani, majani ya giligilani, majani ya minti, pamoja na chumvi, kisha changanya vizuri kwa kutumia uma.

    Step5

    Chukua sufuria dogo lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, iliki, mdalasini, binzari nyembamba, pamoja na pilipili manga, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.

    Step6

    Weka tangawizi, kisha endelea kukaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.

    Step7

    Zima jiko, halafu epua mchanganyiko huo na umimine kwenye kontena lenye mchanganyiko wa viazi, kisha changanya vizuri, tayari kwa kula.

    Conclusion

    Kabla ya kutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.