Jarida la Mapishi

Biringanya za kuponda zenye haradali

Biringanya za kuponda zenye haradali | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 45
  • Walaji
    4

Biringanya za kuponda zenye haradali, ni mboga tamu ambayo hupikwa kwa kutumia biringanya zilizopondwa, adesi, limao, pamoja na viungo vya aina mbalimbali kama vile haradali. Mboga hii yafaa kula pamoja na chapati, wali au mkate. Fuata hatua zifuatazo, ili ukifunze jinsi ya kupika biringanya za kuponda zenye haradali.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Washa jiko la kuoka (oven) na uweke joto la nyuzi 205° C, kisha acha jiko lipate moto. Chukua mafuta ya kupikia na upake kwenye ngozi ya nje ya biringanya, kisha chukua kisu na uchanje sehemu mbali mbali za biringanya hizo kwa kutumia ncha ya kisu.

    Step2

    Weka biringanya ndani ya jiko la kuoka, kisha oka kwa muda wa dakika 30 mpaka 40, au hadi utakapo ona biringanya hizo zimekuwa laini. Ondoa biringanya hizo kutoka kwenye jiko la kuoka na uziweke pembeni ili zipoe.

    Step3

    Menya maganda ya biringanya hizo halafu ziponde vizuri, kisha ziweke kwenye kontena. Weka majani ya giligilani, chumvi, pamoja na limao, halafu changanya vizuri, kisha weka kontena pembeni.

    Step4

    Chukua sufuria ndogo lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka adesi kwenye hilo sufuria, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa sekunde 30.

    Step5

    Weka mbegu za haradali pamoja na majani ya mvuje, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa sekunde kadhaa. Epua na uweke kwenye kontena lenye biringanya, kisha changanga vizuri, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.