Jarida la Mapishi

Mboga ya uyoga na pilipili hoho

Mboga ya uyoga na pilipili hoho | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 20
  • Walaji
    4

Mboga ya uyoga na pilipili hoho, ni pishi tamu kuliko mboga zote za uyoga ulizowahi kula. Mboga ya hii hupikwa kwa kutumia uyoga mbichi, vitunguu, nyanya pamoja na viungo. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mboga hii ya uyoga na pilipili hoho.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kikaango kikubwa chenye mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hicho kikaango, binzari nyembamba pamoja na vitunguu maji, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona vitunguu hivyo vimeiva. Ondoa vitunguu hivyo kutoka kwenye kikaango na uviweke pembeni kwenye kontena.

    Step2

    Weka uyoga kwenye kikaango hicho hicho, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 3 mpaka 5, au hadi utakapo ona uyoga huo umebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia. Ondoa uyoga huo kutoka kwenye kikaango, na uweke pembeni kwenye kontena lenye mchanganyiko wa vitunguu maji.

    Step3

    Weka kwenye kikaango hicho hicho, nyanya, pilipili hoho, tangawizi, pamoja na vitunguu swaumu, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona mchuzi umekuwa mzito.

    Step4

    Weka mbegu za giligilani, chumvi, pamoja na mchanganyiko wa vitunguu maji na uyoga uliomo kwenye kontena, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 3.

    Step5

    Nyunyizia garam masala na ukoroge vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.