Jarida la Mapishi

Mboga ya maharage machanga

Mboga ya maharage machanga | Jarida la Mapishi
 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 20
 • Walaji
  4

Mboga ya maharage machanga, ni mboga nzuri yenye afya na rahisi kupika. Unachohitaji ili kupika mboga hii, ni maharage machanga, vitunguu pamoja na viungo. Ikiwa hujawahi kupika maharage machanga, utafurahia jinsi ilivyo rahisi kupika mboga hii. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mboga hii ya maharage machanga.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, binzari nyembamba pamoja na tangawizi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa sekunde 30.

  Step2

  Ongeza moto na uweke moto mkubwa. Weka maharage machanga, viazi mviringo, mbegu za giligilani, binzari ya manjano, pamoja na chumvi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2 mpaka 3.

  Step3

  Punguza moto na uweke moto wa wastani. Weka nyanya, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 12 mpaka 15, au hadi utakapo ona viazi vimeiva na mchuzi umekuwa mzito.

  Step4

  Weka limao pamoja na garam masala halafu koroga vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *


  The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.