Jarida la Mapishi

Mchuzi wa tanipu

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 35
 • Walaji
  4

Mchuzi wa tanipu, ni mchuzi wenye ladha nzuri ambao hupikwa kwa kutumia mboga ya tanipu, nyanya, pamoja na viungo. Mchuzi huu wa tanipu, wafaa sana kula pamoja na chapati. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mchuzi huu wa tanipu.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, binzari nyembamba, mbegu za kisibiti, pamoja na vitunguu maji, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 7, au hadi utakapo ona vitunguu mani vimeiva.

  Step2

  Weka tangawizi, majani ya tanipu, pamoja na majani ya mvuje, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.

  Step3

  Weka nyanya, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona mchuzi umekuwa mzito.

  Step4

  Weka mbegu za giligilani, binzari ya manjano, chumvi, pamoja na tanipu, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5 zaidi.

  Step5

  Weka maji, halafu koroga vizuri, kisha weka moto mkubwa na uache ichemke.

  Step6

  Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 10 mpaka 15, au hadi utakapo ona tanipu zimekuwa laini na mchuzi umekuwa mzito.

  Step7

  Weka garam masala na ukoroge vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *