Jarida la Mapishi

Magimbi yenye nyanya

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 45
 • Walaji
  4

Magimbi yenye nyanya, ni chakula kitamu na chenye ladha nzuri, ambacho hupikwa kwa kuchanganya magimbi, nyanya pamoja na viungo. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika magimbi haya yenye nyanya.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria, magimbi pamoja na maji, kisha chemsha kwenye jiko lenye moto wa wastani kwa muda wa dakika 20, au hadi utakapo ona magimbi yameiva.

  Step2

  Epua na umwage maji yote yaliyomo kwenye sufuria na kubakiwa na magimbi peke yake, kisha acha yapoe. Magimbi yakishapoa, menya maganda yake yote, kisha yakate katika vipande vidogo vidogo.

  Step3

  Chukua kikaango kikubwa chenye mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hicho kikaango, mbegu za kisibiti, binzari nyembamba, tangawizi, magimbi, pamoja na chumvi, kisha kaanga huku ukiyageuza geuza magimbi mara kwa mara kwa muda wa dakika 10, au hadi utakapo ona magimbi yamebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia. Epua magimbi hayo na uyaweke kwenye kontena.

  Step4

  Weka kwenye kikaango hicho hicho, nyanya, majani ya giligilani, pamoja na vitunguu swaumu, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5 mpaka 7.

  Step5

  Weka vipande vya magimbi ulivyo vikaanga mwanzoni, kisha pika mchanganyiko huo ukivigeuza geuza mara kwa mara vipande hivyo vya magimbi kwa muda wa dakika 3 mpaka 5, au hadi utakapo ona vipande vyote vya magimbi vimechanganyika vyema pamoja na mchanganyiko wa nyanya.

  Step6

  Weka Chaat Masala na ukoroge vizuri, kisha epua na uweke kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *