-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 5
-
Walaji2
Chai ya minti, ni chai ya mitishamba inayotengenezwa kwa kutumia maji, maziwa, tangawizi, pamoja na majani ya minti. Ili kupata ladha nzuri zaidi yachai hii, tengeneza chai hii kwa kutumia majani ya minti aina ya peppermint au spearmint. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza chai hii ya minti.
Ingredients
Directions
Chukua sufuria la ukubwa wa wastani. Weka kwenye hilo sufuria, maji, majani ya minti, pamoja na tangawizi, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa.
Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, kisha acha iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 1.
Mimina maziwa halafu koroga vizuri, kisha acha ichemke.
Ukiona imechemka, weka majani ya chai halafu koroga tena vizuri, kisha zima jiko.
Epua na uweke pembeni, kisha funika sufuria na uache itulie kwa muda wa dakika 3.
Chukua vikombe 2 pamoja na chujio. Chuja chai ndani ya hivyo vikombe. Weka sukari au asali kadiri ya mahitaji yako, kisha koroga vizuri, tayari kwa kunywa.
Leave a Review