Jarida la Mapishi

Lemonade ya raspberry na minti

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  -
 • Walaji
  2

Lemonade ya raspberry na minti, ni kinywaji rahisi kutengeneza, chenye ladha nzuri na cha kuburudisha, ambacho hutengenezwa kwa kusaga pamoja matunda ya raspberry, limao, majani ya minti, maji na sukari. Kinywaji hiki chafaa sana kunywa katika msimu wa kiangazi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza lemonade hii ya raspberry na minti.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, malimao, matunda ya apple, matunda ya raspberry, majani ya minti, maji, pamoja na sukari, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.

  Step2

  Chukua chujio, kisha chuja lemonade hiyo vizuri.

  Step3

  Mimina lemonade kwenye chombo safi, kisha iweke kwenye friji ili ipate baridi, kabla ya kunywa.

  Conclusion

  Unaweza kuongeza maji zaidi, endapo utaona maji yaliyomo katika lemonade hii ni kidogo.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *